Sunday, August 27, 2017

Jinsi ya Kumgundua Mtu Anaye Danganya kwa Haraka


Ukweli ni kuwa watu hudanganya sana zaidi ya wana vyosema ukweli, kwa mujibu wa mwanishi wa kitabu cha The Day America Told the Truth asilimia 91 ya watu hudanganya wakiwa kazini au nyumbani.Sasa basi najua hakuna anayependa kudanganywa lakini ikitokea umehisi umedanganywa basi hizi ndizo njia ambazo unaweza kumgundua mtu muongo kwa haraka.
  • Muongo Huwa Anakuwa Yuko Siriaz Sana Anapo Danganya
Kwa mujibu wa wataalamu wa saikolojia hii ni ishara kubwa sana kwa mtu muongo kwani hufanya hivi ili kukupa nafasi ya wewe kumuamini kutokana na kuwa kwake sirias, lakini pia mara chache watu wengine waongo hucheka wanapo danganja.
  • Kushika Maeneo ya Uso Mara Nyingi
Watu wengi waongo wakati wanasema uongo hujikuta wanashika uso mara nyingi sana, hii huwa ni kitendo ambacho huja gafla na huwa mtu muongo hawezi kujizuia.
  • Kushika Pua Mara Nyingi
Hii ni tabia ya watu wengi sana waongo kwani hujikuta wanashika poa mara nyingi sana, yani kuliko kawaida. Hii huja gafla na unaweza kudhani huyo mtu amepatwa na mafua lakini ni vyema ukagundua kama huyo mtu ana mafua kwanza maana usije ukachanganya kati ya mtu muongo na mwenye mafua.
  • Husugua Macho Mara Nyingi
Mara nyingi watu waongo huwa hawataki kukuangalia usoni wakati wa kudanganya hivyo kama ikitokea mtu muongo amekudanyanga na mlikua macho kwa macho utanza kuona anakwepesha macho huku akiyasugua ili kupoteza eye contact.

Na hizo ni baadhi ya njia tu ambazo unaweza kutumia kuweza kumtambua muongo, kumbuka kuwa mara nyingi ili kumgundua muongo unatakiwa usiwe mtu wa papara kuwa mpole na kuwa mtulivu na angalia lugha ya mtaendo au kingereza inaitwa "Body Language" ukiweza hili utakuwa na njia rahisi ya kuweza kumjua mtu muongo.

Tuesday, August 15, 2017

Jinsi ya Kujua Kiwango cha Mwisho cha Umeme Kwenye Luku


Kwa kuanza basi nadhani kila mtu atakua anaijua mita ya Luku jinsi ilivyo pamoja na muonekano wake pale unapo ingiza tarakimu ili kuweka umeme, pia najua mita zinatofautiana lakini naimani njia hii inafanya kazi karibia kwa kila mita za Luku ambazo zinatumia vibonyezo vya namba.

Basi kama mita yako iko hivyo moja kwa moja ili kuangalia kiwango cha umeme kwenye mita yako hakikisha kuna umeme kisha bofya namba 2 pamoja na kibonyezo cha kuweka umeme (Enter) hakikisha unabonyeza vyote kwa pamoja kisha achia.



Baada ya hapo utaona namba za kwanza ambazo ndizo zinaonyesha kiwango cha umeme kilicho wekwa kwa mara ya mwisho kwenye mita yako ya Luku, hakikisha unaangalia namba za kwanza zinazo anza kutokea kwenye kioo cha mita yako kwani namba hizo hubadilika na baadae baada ya kama sikunde 3 namba hizo hurudia hali yake ya awali na kuendelea kuhesabu kiwango cha umeme uliopo hivyo kama utakua ujaona vizuri basi subiria namba hizo zirudi kwenye hali yake alafu urudie tena kufanya hatua hizo.

Angalizo : Njia hii ni salama kabisa lakini kumbuka Mita ya Luku ni mali ya Tanesco hivyo ni vyema kufanya hatua hizi kwa uangalifu usije kuharibu au kubadili chochote kwenye mfumo wa mita yako.

Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kungalia kiwango cha mwisho kilichowekwa kwenye mita yako ya Luku

Imetoka : Tanzania Tech

Video : Jinsi ya Kumenya Mayai ya Kuchemsha kwa Haraka


Kuna wakati unataka kula mayai ya kuchemsha Asubuhi kabla ujaenda kazini, lakini ukifikiria ule ugumu unaokuja hasa kwenye kumenya maganda ya mayai hayo basi unajikuta unaona uvivu na kukosa virutubisho kibao vinavyo patikana kwenye mayai ya kuchemsha.

Basi kama umekuaunakosa kula mayai sababu ya kupata uvivu wa kumenya basi hii ni kwaajili yako. Chakufanya baada ya kumaliza kuchamsha mayai yako chukua kikombe cha plastiki kisha weka yai lako ndani yake kisha weka maji ya kawaida kisha funika alafu tingisha kwa muda kisha toa yai lako utaona lina menyeka kirahisi kabisa.

Jinsi ya Kuhifadhi Ndizi za Kuiva Zisiharibike


Linapokuja swala la chakula wengi wetu hatuna maujanja kiasi kwamba tunakosa ujuzi na kujikuta tunatupa chakula kila siku, lakini kupitia maujanja.com tutajifunza mbinu mbalimbali za kukusaidia kuboresha maisha yako pamoja na chakula unachokula.

Baada ya kusema hayo basi leo twende tukajifunze maujanja ya kuhidhi ndizi za kuiva ili zisiharibike au kuoza. Wote tunajua kuwa ndizi ya kuiva iki kaa kwa muda mrefu bila kuliwa basi upata mabaka mabaka meusi na baadae kuharibika.

Lakini unaweza kusia yote hayo kwa kufanya maujanja haya ambayo nauhakika yatakusaidia sana. Chakufanya unapo nunua chips usitupe lile foili bali lisafishe vizurina ulikaushe kabisa kisha chaukua ndizi zako za kuiva ambazo bado ziko kwenye kikonyo kisa zungushia foili kwenye sehemu ya kikonyo na uhakikisha umeifunika yote..

Baada ya kufanya yote hayo basi utaona ndizi zako za kuiva zikiwa na uwezo wa kukaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika, yaani zinaweza kukaa hata zaidi ya siku saba kama eneo ulilopo halina joto sana.

Jinsi ya Kuomba Hela kwa Mtu Ili Akupe Kirahisi


Wote tumeshawahi kupitia kwenye ile hatua ya kuomba hela iwe wewe ni mtoto au hata mtu mzima ukweli ni kuwa tabia hii haizuiliki. Ndio maana leo nina kupa maujanja jinsi ya kuomba hela na ukapewa moja kwa moja.

Ukweli ni kwamba kuombwa hela wakati mwingine ni kero sana na hii usababisha wakati mwingine kukuta mtu ana kutamkia maneno ya kero na kumfanya mtu anae omba hela kusikia vibaya lakini leo nina maujanja juu ya hili.

Bila kupoteza muda njoo nikufundishe, kumbuka unapo omba hela kuwa na sababu ya msingi kutokana na aina ya mtu unaye kwenda kumuomba kwa mfano kama ni baba uwe na sababu ambayo unajua baba ataelewa na kama ni mama vivyo hivyo. sababu zinaweza kutofautiana kutokana na aina ya mtu na tabia zake.

Kama umesha pata sababu basi uko tayari kwa maujanja haya. Sasa basi pale unapotaka kuomba hela ni vyema sana kuomba kiasi kikubwa yaani hapa na maanisha kuomba zaidi ya lengo lako, alafu mtu unayemuomba akikukatalia basi omba kela kiwango ambacho ulidhamiria kuomba, hii inafanya kazi muda wote.. niamini.

Yaani kwa mfano unashida ya elfu kumi, pale unapoenda kumuomba mtu usimuombe elfu kumi bali omba hata elfu thelathini na endapo mtu huyu amekataa basi sasa omba kile kiwango chako yaani mwambie "basi naomba hata elfu kumi itanisaidia"mara moja mtu huyu atakuwa yuko tayari kukupa hii ndogo kulingana na shida yako... Vipi maujanja haya yamekusaidia..?

Video : Jinsi ya Kujua Aina za Plastic na Matumizi Yake


Wote tunatumia vifaa vya plastiki na kati yetu plastiki pia ni sehemu muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku, hivyo basi ni vyema leo kujua siri ambazo ulikua hujui zilizoko chini ya vifaa vya plastik.

Ukweli ni kwamba kila plastiki unayo iona imetengenezwa kwa aina tofauti ya plastiki, aina hizo zimetengenezwa maalum ili kudhibiti ubora wa kitu kilichopo ndani ya plastiki au wakati mwingine zinatengenezwa hivyo ili kuwezesha matumizi bora ya kifaa hicho.. hivyo basi zifuatazo ni aina za plastiki ambazo hutakiwi kutumia mara mbili.


Maelezo zaidi ni kuwa, ni muhimu kuwa makini unapotumia plastiki ni bora kuwa makini kwa kuangalia aina ya alama ambazo zinapatikana chini ya plastiki ili kujua kama unaweza kutumia plastiki hiyo kwa mara ya pili.

Ni vyema kuwa makini na chupa au vyombo vya plastiki vyenye alama za pembe tatu na maandishi ya V kisha 3 kwenye pembe tatu, PS kisha 6 kwenye pembe tatu, pamoja na OTHER kisha 7 kwenye pembe tatu kwani vyombo hivi havifai kwa matumizi ya kuweka vyakula au maji, lakini pia kumbuka chupa au vyombo vya plastiki vyenye alama za PETE kisha 1 kwenye pembe kwani hivi inaruhusiwa kutumika mara moja na sio zaidi kwani vyombo hivi vikipata Oxygen au vikipigwa na jua kwa muda huweza kutoa kemikali zinazoweza kuadhiri afya yako.

Kwa matumizi salama ya vyombo vya plastiki ni vyema kuangalia vyombo vyenye alama za HDPE kisha 2 kwenye pembe tatu, LDPE kisha 4 kwenye pembe tatu, pamoja na PP kisha 5 kwenye pembe tatu, vifaa hivi ni salama kabisa kwa kutumia mara zaidi ya moja lakini kumbuka ni vyema uwe unaviosha kwa umakini na kwa kutumia sabuni maalum.

Nimeona ni bora nikufahamishe hii kwani aina hizi za plastiki ndizo tunazo tumia kila siku hivyo nimeona ni muhimu sana wewe kuweza kujua hili ili kuweza kujilinda kwani wengi wetu hatuna ustarabu wa kuangalia alama hizi pale tunapo nunua vifaa au vyombo hivi tena hasa vile ambavyo tunatumia kwa matumizi ya kula ama kunywa.. Hope this help!!

Saturday, August 12, 2017

Jinsi ya Kutakatisha Zaidi Sinki la Choo Chako Nyumbani


Wote tunajua magonjwa yanayo sababishwa na choo kuwa kichafu, lakini mbali na magonjwa ukweli ni kwamba choo kichafu au kilicho fubaa akivutii kabisa. Kama hili ni tatizo kwako basi soma hii.

Kama choo chako ni cha sink na kimefubaa kwa uchafu wa kahawia ambao ni mgumu kutoka basi huna haja ya kwenda kununua madawa ya bei ghali ambayo pengine yanaweza yasisaidie, bali sasa fuata hatua hizi rahisi.

Hatua ya kwanza osha choo chako vizuri kisha nenda dukani kwa mangi... na nunua chupa moja ya Coca cola kisha nyunyuzia pembeni ya choo hakikisha kiala sehemu ya sinki imepata kisha acha ndani ya dakika 15 kisha osha choo chako kwa brashi gumu lenye kusugua kwa muda kama dakika 1 au 2 kisha osha choo chako na maji safi.

Hapo utafaikiwa kufanya choo chako kungaa sana na ni matumaini yangu utaendelea kutumia maujanja haya kila mara kufanya choo chako kungara na kuvuti wageni wako.

Jinsi ya Kujua Kama Mayai ni Mazima au Mabovu


Kuna njia nyingi sana za kufuata kujua kama chakula ni kibovu au kizima, lakini kwa upande wa mayai vilevile kuna njia nyingi za kufuata lakini njia hii ifuatayo ni bora sana kwa nyumbani.

Njia ifuatayo ni bora sana kama umehifadhi mayai nyumbani na ungependa kujua kama ni mazima au mabovu biala hata kuyapasua ili kuepukana na harufu kali inayotokana na mayai mabovu. Ngooja kwanza najua hapa utafikiri kuwa njia hii ni ile ya kuangalia mayai kwenye mwanga... no... hapana.

Kwenye hatua hii unahitaji bakuli kubwa la maji kisha jaza maji mpaka juu, kisha anza kudumbukiza mayai moja baada ya lingine. Kama yai limezama mpaka mwisho wa bakuli basi jua kuwa yai hilo ni zima na kama ukiona yai lina elea juu-juu basi jua kuwa yai ilo ni bovu...

Pia kumbuka kama yai limezama kiasi na kuishia katikati jua kuwa yai hilo sio zima sana maana yake ni kuwa yai hilo limeanza kuharibika hivyo ni vyema ukatupa yai hilo pia.

Uzuri wa njia hii ni kuwa unaweza kutambua mayai kama ni mabovu kwa pamoja yaani ukiwa na bakuli kubwa unadumbukiza mayai yote kisha yale yatakayo panda juu basi hayo yatakuwa sio mazima, Hii itakusaidia kurahisisha kazi hata kwako muuza duka.

Jinsi ya Kungarisha Ngozi Yako kwa Haraka kwa Vitu Halisi


Ni mara nyingi sana tumesha sikia watu wakiadhirika na vipodozi mbalimbali na yote hii inasbabishwa na watu hao kutaka kungarisha ngozi zao kwa kutumia vipodozi hivyo.

Ifuatayo ni njia ambayo itakusaidia kufanya ngozi yako kungara na kukuacha ukiwa na weupe au weusi wako wa asili pamoja na ngizi nyororo.

Hatua ya kwanza unaitaji mahitaji yafuatayo, unahitaji asali vijiko viwili vya chakula, pia unahitaji sukari kijiko kimoja cha chakula na pia unahitaji nusu kipande cha chungwa pamoja na nusu kipande cha limao.

Kwa kuanza kwa uangalifu chukua bakuli na changanya asali pamoja na sukari kisha kamulia juice ya nusu kipande cha chungwa kisha changanya mchanganyiko ho vizuri changanya kwa dakika kama 10 au 15 kisha chukua kipande cha limao kisha dumbukiza kwenye mchanganyiko huo kisha anza kujipaka kwa kutumia kipande hicho.

Jinsi ya Kufanya Simu ya iPhone Kujaa Chaji kwa Haraka


Kuna wakati kuchaji simu yako ya iphone mpaka ijae kabisa inakuwa ni mthiani mkubwa sana na kwa bahati mbaya zaidi iphone nyingi hazina teknolojia ya fast charging hivyo kufanya simu yako kuchelewa sana kujaa chaji. lakini kwa kutumia njia hizi utaweza kufanya simu yako kujaa chaji kwa haraka zaidi kuliko inavyokua kawaida, Basi moja kwa moja twende tukangalie njia hizi.
  • Chaji kwa Kutumia Chaji ya iPad
Kama unayo iPad basi lazima pia utakuwa unayo chaji yake, kama unayo basi tumia chaji hiyo yenye wattage 10W au 12W kuchaji iphone yako hii itakusaidia kuliko kutumia chaji ya iPhone ambayo inatumia 5W.
  • Washa Flight Mode Unapokua Unachaji Simu
Mara nyingi simu yako ya iphone inatumia chaji kutokana na vitu mbalimbali ambavyo vinakua bado vinafanya kazi, lakini pale unapoweka Flight Mode umeme unaoingia kwenye simu yako unakuwa hautumiki kwa vyvovyote zaidi ya kuchaji battery ya simu yako, hivyo flight mode husaidia sana.

Soma zaidi hapa >> Jinsi ya Kufanya Simu ya iPhone Kujaa Chaji kwa Haraka

Jinsi ya Kuhifadhi Karoti Ziwe Fresh Kwenye Jokofu


Wote tunajua kuwa kuna wakati unataka kuhitaji kutumia karoti zilizoko kwenye jokofu lakini unashangaa paleunapofungua frige na kukuta karoti hizo zimekauka.

Kama hili lilikuwa likikusumbua basi ifuatayo ni njia mbayo itakusaidia wewe kuweza kuhifadhi karoti zako kwenye jokufu ili ziwe kwenye hali nzuri kama vile zimetoka shambani muda huo.

Basi hatua ya kwanza hakikisha unaosha karoti zako vizuri kisha chukua bakuli zuri la plastick amabalo unajua litaweza kutosha karoti zako kisha dumbukiza karoti zako kwenye bakuli hilo au plastiki hiyo kisha weka maji mpaka karoti zote ziwe zimefunikwa kabisa na maji.

Baada ya hapo sasa weka karoti zako kwenye jokofu lako, kumbuka usifunike karoti hizo bali ziache zikiwa kwenye maji ndani ya jokofu... Hapo utakuwa umehifadhi karoti zako vizuri na hapo utakuwa ukitaka kutumia karoti zako zitakuwa fresh kabisa kama zimetoka shambani...