
Linapokuja swala la chakula wengi wetu hatuna maujanja kiasi kwamba tunakosa ujuzi na kujikuta tunatupa chakula kila siku, lakini kupitia maujanja.com tutajifunza mbinu mbalimbali za kukusaidia kuboresha maisha yako pamoja na chakula unachokula.
Baada ya kusema hayo basi leo twende tukajifunze maujanja ya kuhidhi ndizi za kuiva ili zisiharibike au kuoza. Wote tunajua kuwa ndizi ya kuiva iki kaa kwa muda mrefu bila kuliwa basi upata mabaka mabaka meusi na baadae kuharibika.
Lakini unaweza kusia yote hayo kwa kufanya maujanja haya ambayo nauhakika yatakusaidia sana. Chakufanya unapo nunua chips usitupe lile foili bali lisafishe vizurina ulikaushe kabisa kisha chaukua ndizi zako za kuiva ambazo bado ziko kwenye kikonyo kisa zungushia foili kwenye sehemu ya kikonyo na uhakikisha umeifunika yote..
Baada ya kufanya yote hayo basi utaona ndizi zako za kuiva zikiwa na uwezo wa kukaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika, yaani zinaweza kukaa hata zaidi ya siku saba kama eneo ulilopo halina joto sana.