
Kuna njia nyingi sana za kufuata kujua kama chakula ni kibovu au kizima, lakini kwa upande wa mayai vilevile kuna njia nyingi za kufuata lakini njia hii ifuatayo ni bora sana kwa nyumbani.
Njia ifuatayo ni bora sana kama umehifadhi mayai nyumbani na ungependa kujua kama ni mazima au mabovu biala hata kuyapasua ili kuepukana na harufu kali inayotokana na mayai mabovu. Ngooja kwanza najua hapa utafikiri kuwa njia hii ni ile ya kuangalia mayai kwenye mwanga... no... hapana.
Kwenye hatua hii unahitaji bakuli kubwa la maji kisha jaza maji mpaka juu, kisha anza kudumbukiza mayai moja baada ya lingine. Kama yai limezama mpaka mwisho wa bakuli basi jua kuwa yai hilo ni zima na kama ukiona yai lina elea juu-juu basi jua kuwa yai ilo ni bovu...
Pia kumbuka kama yai limezama kiasi na kuishia katikati jua kuwa yai hilo sio zima sana maana yake ni kuwa yai hilo limeanza kuharibika hivyo ni vyema ukatupa yai hilo pia.
Uzuri wa njia hii ni kuwa unaweza kutambua mayai kama ni mabovu kwa pamoja yaani ukiwa na bakuli kubwa unadumbukiza mayai yote kisha yale yatakayo panda juu basi hayo yatakuwa sio mazima, Hii itakusaidia kurahisisha kazi hata kwako muuza duka.