
Ni mara nyingi sana tumesha sikia watu wakiadhirika na vipodozi mbalimbali na yote hii inasbabishwa na watu hao kutaka kungarisha ngozi zao kwa kutumia vipodozi hivyo.
Ifuatayo ni njia ambayo itakusaidia kufanya ngozi yako kungara na kukuacha ukiwa na weupe au weusi wako wa asili pamoja na ngizi nyororo.
Hatua ya kwanza unaitaji mahitaji yafuatayo, unahitaji asali vijiko viwili vya chakula, pia unahitaji sukari kijiko kimoja cha chakula na pia unahitaji nusu kipande cha chungwa pamoja na nusu kipande cha limao.
Kwa kuanza kwa uangalifu chukua bakuli na changanya asali pamoja na sukari kisha kamulia juice ya nusu kipande cha chungwa kisha changanya mchanganyiko ho vizuri changanya kwa dakika kama 10 au 15 kisha chukua kipande cha limao kisha dumbukiza kwenye mchanganyiko huo kisha anza kujipaka kwa kutumia kipande hicho.