Saturday, August 12, 2017

Jinsi ya Kufanya Simu ya iPhone Kujaa Chaji kwa Haraka


Kuna wakati kuchaji simu yako ya iphone mpaka ijae kabisa inakuwa ni mthiani mkubwa sana na kwa bahati mbaya zaidi iphone nyingi hazina teknolojia ya fast charging hivyo kufanya simu yako kuchelewa sana kujaa chaji. lakini kwa kutumia njia hizi utaweza kufanya simu yako kujaa chaji kwa haraka zaidi kuliko inavyokua kawaida, Basi moja kwa moja twende tukangalie njia hizi.
  • Chaji kwa Kutumia Chaji ya iPad
Kama unayo iPad basi lazima pia utakuwa unayo chaji yake, kama unayo basi tumia chaji hiyo yenye wattage 10W au 12W kuchaji iphone yako hii itakusaidia kuliko kutumia chaji ya iPhone ambayo inatumia 5W.
  • Washa Flight Mode Unapokua Unachaji Simu
Mara nyingi simu yako ya iphone inatumia chaji kutokana na vitu mbalimbali ambavyo vinakua bado vinafanya kazi, lakini pale unapoweka Flight Mode umeme unaoingia kwenye simu yako unakuwa hautumiki kwa vyvovyote zaidi ya kuchaji battery ya simu yako, hivyo flight mode husaidia sana.

Soma zaidi hapa >> Jinsi ya Kufanya Simu ya iPhone Kujaa Chaji kwa Haraka