Saturday, August 12, 2017

Jinsi ya Kuhifadhi Karoti Ziwe Fresh Kwenye Jokofu


Wote tunajua kuwa kuna wakati unataka kuhitaji kutumia karoti zilizoko kwenye jokofu lakini unashangaa paleunapofungua frige na kukuta karoti hizo zimekauka.

Kama hili lilikuwa likikusumbua basi ifuatayo ni njia mbayo itakusaidia wewe kuweza kuhifadhi karoti zako kwenye jokufu ili ziwe kwenye hali nzuri kama vile zimetoka shambani muda huo.

Basi hatua ya kwanza hakikisha unaosha karoti zako vizuri kisha chukua bakuli zuri la plastick amabalo unajua litaweza kutosha karoti zako kisha dumbukiza karoti zako kwenye bakuli hilo au plastiki hiyo kisha weka maji mpaka karoti zote ziwe zimefunikwa kabisa na maji.

Baada ya hapo sasa weka karoti zako kwenye jokofu lako, kumbuka usifunike karoti hizo bali ziache zikiwa kwenye maji ndani ya jokofu... Hapo utakuwa umehifadhi karoti zako vizuri na hapo utakuwa ukitaka kutumia karoti zako zitakuwa fresh kabisa kama zimetoka shambani...