
Matangazo au (Ads) kwenye programu au application ndio chanzo pekee kinacho msaidia mtu kupata kipato kupitia programu yake tena zaidi ni pale unapokuta programu hiyo ni ya bure au (Free), lakini matangazo hayo yakizidi sana yanapoteza ladha ya kutumia programu hiyo na pengine kukufanya kuamua kuacha kabisa kutumia programu hiyo. Kutokana na hilo leo Tanzania Tech tunakuletetea njia hii ya kupunguza matangazo hayo na pengine kuyatoa kabisa kutoka kwenye programu zako za mfumo wa Android.
Kwa kuanza basi ningependa tu kusema kuwa njia hii inaweza kuondoa kabisa matangazo au kupunguza na kwa namna moja ama nyingine kuna wakati unaweza usione matokeo moja kwa moja lakini na uhakika itakusaidia hata kupunguza matangazo hayo. Kwa kuanza unatakiwa kudownload programu inayoitwa Lucky Patcher unaweza kudownload kupitia hapa baada ya kudownload install progarmu hiyo kama bado hakikisha unaweka tiki kwenye Setting > Security > kisha weka tiki palipo andikwa "Unknown sources" alafu maliza kwa kubofya OK endelea mbele kwa kufungua programu hiyo.
Baada ya Kufungua programu hiyo hakikisha unaacha kwanza imalize kutafuta programu zote na pia kama kuna update za programu hiyo hakikisha una update kwani kwa kufanya hivyo uwezekano wa programu hiyo kufanya kazi unakuwa mkubwa zaidi. Baada ya kumaliza kutafuta utaona programu zote ambazo ziko kwenye simu yako, tafuta programu unayotaka kuondoa matangazo kisha ichague kwa kuibofya alafu chagua Open Menu Patches kisha bofya tena Create Modified APK File kisha chagua APK without Google Ads kisha chagua Rebulid App iliyoko mwisho kabisa wa programu hiyo
Soma zaidi hapa >> Jinsi ya Kuondoa Matangazo Kwenye Programu za Android