
Wote tumeshawahi kupitia kwenye ile hatua ya kuomba hela iwe wewe ni mtoto au hata mtu mzima ukweli ni kuwa tabia hii haizuiliki. Ndio maana leo nina kupa maujanja jinsi ya kuomba hela na ukapewa moja kwa moja.
Ukweli ni kwamba kuombwa hela wakati mwingine ni kero sana na hii usababisha wakati mwingine kukuta mtu ana kutamkia maneno ya kero na kumfanya mtu anae omba hela kusikia vibaya lakini leo nina maujanja juu ya hili.
Bila kupoteza muda njoo nikufundishe, kumbuka unapo omba hela kuwa na sababu ya msingi kutokana na aina ya mtu unaye kwenda kumuomba kwa mfano kama ni baba uwe na sababu ambayo unajua baba ataelewa na kama ni mama vivyo hivyo. sababu zinaweza kutofautiana kutokana na aina ya mtu na tabia zake.
Kama umesha pata sababu basi uko tayari kwa maujanja haya. Sasa basi pale unapotaka kuomba hela ni vyema sana kuomba kiasi kikubwa yaani hapa na maanisha kuomba zaidi ya lengo lako, alafu mtu unayemuomba akikukatalia basi omba kela kiwango ambacho ulidhamiria kuomba, hii inafanya kazi muda wote.. niamini.
Yaani kwa mfano unashida ya elfu kumi, pale unapoenda kumuomba mtu usimuombe elfu kumi bali omba hata elfu thelathini na endapo mtu huyu amekataa basi sasa omba kile kiwango chako yaani mwambie "basi naomba hata elfu kumi itanisaidia"mara moja mtu huyu atakuwa yuko tayari kukupa hii ndogo kulingana na shida yako... Vipi maujanja haya yamekusaidia..?