
Wote tunajua magonjwa yanayo sababishwa na choo kuwa kichafu, lakini mbali na magonjwa ukweli ni kwamba choo kichafu au kilicho fubaa akivutii kabisa. Kama hili ni tatizo kwako basi soma hii.
Kama choo chako ni cha sink na kimefubaa kwa uchafu wa kahawia ambao ni mgumu kutoka basi huna haja ya kwenda kununua madawa ya bei ghali ambayo pengine yanaweza yasisaidie, bali sasa fuata hatua hizi rahisi.
Hatua ya kwanza osha choo chako vizuri kisha nenda dukani kwa mangi... na nunua chupa moja ya Coca cola kisha nyunyuzia pembeni ya choo hakikisha kiala sehemu ya sinki imepata kisha acha ndani ya dakika 15 kisha osha choo chako kwa brashi gumu lenye kusugua kwa muda kama dakika 1 au 2 kisha osha choo chako na maji safi.
Hapo utafaikiwa kufanya choo chako kungaa sana na ni matumaini yangu utaendelea kutumia maujanja haya kila mara kufanya choo chako kungara na kuvuti wageni wako.