Sunday, August 27, 2017

Jinsi ya Kumgundua Mtu Anaye Danganya kwa Haraka


Ukweli ni kuwa watu hudanganya sana zaidi ya wana vyosema ukweli, kwa mujibu wa mwanishi wa kitabu cha The Day America Told the Truth asilimia 91 ya watu hudanganya wakiwa kazini au nyumbani.Sasa basi najua hakuna anayependa kudanganywa lakini ikitokea umehisi umedanganywa basi hizi ndizo njia ambazo unaweza kumgundua mtu muongo kwa haraka.
  • Muongo Huwa Anakuwa Yuko Siriaz Sana Anapo Danganya
Kwa mujibu wa wataalamu wa saikolojia hii ni ishara kubwa sana kwa mtu muongo kwani hufanya hivi ili kukupa nafasi ya wewe kumuamini kutokana na kuwa kwake sirias, lakini pia mara chache watu wengine waongo hucheka wanapo danganja.
  • Kushika Maeneo ya Uso Mara Nyingi
Watu wengi waongo wakati wanasema uongo hujikuta wanashika uso mara nyingi sana, hii huwa ni kitendo ambacho huja gafla na huwa mtu muongo hawezi kujizuia.
  • Kushika Pua Mara Nyingi
Hii ni tabia ya watu wengi sana waongo kwani hujikuta wanashika poa mara nyingi sana, yani kuliko kawaida. Hii huja gafla na unaweza kudhani huyo mtu amepatwa na mafua lakini ni vyema ukagundua kama huyo mtu ana mafua kwanza maana usije ukachanganya kati ya mtu muongo na mwenye mafua.
  • Husugua Macho Mara Nyingi
Mara nyingi watu waongo huwa hawataki kukuangalia usoni wakati wa kudanganya hivyo kama ikitokea mtu muongo amekudanyanga na mlikua macho kwa macho utanza kuona anakwepesha macho huku akiyasugua ili kupoteza eye contact.

Na hizo ni baadhi ya njia tu ambazo unaweza kutumia kuweza kumtambua muongo, kumbuka kuwa mara nyingi ili kumgundua muongo unatakiwa usiwe mtu wa papara kuwa mpole na kuwa mtulivu na angalia lugha ya mtaendo au kingereza inaitwa "Body Language" ukiweza hili utakuwa na njia rahisi ya kuweza kumjua mtu muongo.