
Kwa kuanza basi nadhani kila mtu atakua anaijua mita ya Luku jinsi ilivyo pamoja na muonekano wake pale unapo ingiza tarakimu ili kuweka umeme, pia najua mita zinatofautiana lakini naimani njia hii inafanya kazi karibia kwa kila mita za Luku ambazo zinatumia vibonyezo vya namba.
Basi kama mita yako iko hivyo moja kwa moja ili kuangalia kiwango cha umeme kwenye mita yako hakikisha kuna umeme kisha bofya namba 2 pamoja na kibonyezo cha kuweka umeme (Enter) hakikisha unabonyeza vyote kwa pamoja kisha achia.

Baada ya hapo utaona namba za kwanza ambazo ndizo zinaonyesha kiwango cha umeme kilicho wekwa kwa mara ya mwisho kwenye mita yako ya Luku, hakikisha unaangalia namba za kwanza zinazo anza kutokea kwenye kioo cha mita yako kwani namba hizo hubadilika na baadae baada ya kama sikunde 3 namba hizo hurudia hali yake ya awali na kuendelea kuhesabu kiwango cha umeme uliopo hivyo kama utakua ujaona vizuri basi subiria namba hizo zirudi kwenye hali yake alafu urudie tena kufanya hatua hizo.
Angalizo : Njia hii ni salama kabisa lakini kumbuka Mita ya Luku ni mali ya Tanesco hivyo ni vyema kufanya hatua hizi kwa uangalifu usije kuharibu au kubadili chochote kwenye mfumo wa mita yako.
Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kungalia kiwango cha mwisho kilichowekwa kwenye mita yako ya Luku
Imetoka : Tanzania Tech